google ads

YAMEKUKUTA VANESA

  

YAMEKUKUTA  VANESA

Na,Joshua shao

0622186752 SMS/CALL

0713111547 WHATSAPP TU

Harufu ya marashi yake Ilimfanya kila mtu kugeuka kumtazama aliyekuwa anapita ni nani ,wanawake na vijana walipata shida sio kidogo kwani kila mmoja aliishiwa na nguvu ya kumsemesha Vanesa kutokana na  alivyokuwa akijiweka

Vanesa ni msichana mwenye umri wa miaka 23 alimaliza masomo yake ya elimu ya juu akiwa na umri mdogo sana hii ni kutokana na kuwaishwa shule ,aliwaishwa shule kutokana na uwezo wake wa kufikiri kuwa mkubwa sana ,sio tu waalimu wake kila mahali walimsifia sana Vanesa kwani alikuwa na akili kupindukia Mbali na uzuri aliokuwa nao Vanesa alikuwa na sura nzuri yenye kuvutia na kutamanisha kila mtu aliyekuwa akimwona alikuwa akitamani kumtazama tu  bila kuchoka hii ni kutokana na uzuri usio na kifani aliokuwa nao Vanesa,.Vanesa alilitambua hili ,mwanzoni alichukulia kawaida ila alipoanza kukua hali ya kujisifu ilianza kukua na kufika juu ,Vanesa alimdharau kila mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa akitamani kusifiwa yeye tu kila akiona mtu anamsifia mwanamke mwingine alikuwa akisunya na kusema ``Wapi Yule mnasema mzuri kwa lipiiiii??’’ hakika Vanesa alikumbwa na roho ya ajabu sana kiasi cha kujishangaa hadi mwenyewe

Baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu ya uhasibu Vanes aliingia katika ulimwengu wa kusaka ajira ,alizunguka sehemu mbalimbali kutafuta ajira alipeleka barua zake takribani ofisi tano ,cha kushangaza ofisi zote zilimkubalia Vanesa jambo ambalo lilimpa kiburi sana na kujiona yeye ni wa tofauti

Vanesa baada ya kufikiria sana aliamua kuelekea kwenye kampuni ya kitalii ambayo aliomba kazi ya uhasibu ,siku ya kwanza alipofika walimwitaji kwa ajili ya kumhoji maswali machache na kupanga juu ya mshahara ,vanesa alipofika aliitwa na meneja wa kampuni hiyo aliulizwa maswali mbali mbali ,hadi meneja alishangaa ni uwezo wa jinsi gani aaliokuwa nao binti Yule kwani alijibu maswali yale kifasaha sana na kwa umakini ,meneja alimwambia

``Unaonaje tukaanza kukulipa laki tisa baada ya muda tukakulipa milioni moja kama mshahara wako wa moja kwa moja ‘’

Vanesa alisimama na kusunya kwa dharau kisha aliondoka huku akisema

``Laiti kama ningejua nisingekuja hapa kupoteza muda na nyie mnanitia laki tisa mimi khaaa hii ni bei ya hili begi langu nimenunua hili begi dola 700 za kimarekani ‘’

Meneja alisema

``Binti tutakuongezea tutaafanya milioni na laki mbili”

Vanesa wala hakugeuka nyuma alipitiliza kwa madoido yote na kuondoka hakuwa na muda wa kusubiri 

Ilipofika jumatatu asubuhi Vanesa aliamkia katika supermarket kubwa ambayo aliomba pia kazi ya uhasibu, alipofika alikaribishwa kwa meneja ,supermarket ile ilikuwa ni kubwa sana kwani wageni mbalimbali kutoka nchi za nje walishukia hapo kwa manunuzi

Meneja alimhoji Vanesa na kumwambia

``Unaonaje tukikupatia shilingi milioni tatu kama mshahara wa kuanzia ‘’

Vanesa alijishauri na kusema

``Hakutakuwa na neno ‘’

Vanesa aliitwa nje na kukabidhiwa funguo ya gari ,wafanyakazi wa kampuni hiyo ya mauzo wote walipewa magari ya kutembelea na kuja kazini

Vanesa akiwa amevalia kama malkia elizabeti alipanda ndani ya gari kali aliweka mkono pembeni kisha akaliwasha na kumwaga meneja kwa kumwambia kuwa kesho ndio ataanza kazi

Meneja alimpungia ,Vanesa huyooo aliondoka zake ,meneja alijivunia na kusema

``Hakika tumempata mwanamke mwenye uwezo mkubwa sana hapa kazini ,mwanamke anayeweza kupiga mahesabu ya mamilioni kwa kutumia kichwa chake bila ya Mashine,naiona kampuni yetu ikikuwa vyema.

Ilipofika asubuhi shughuli zilianza ndani ya supermarket kubwa ya Arusha kila mmoja alikuwa akichacharika majira ya saa mbili Vanesa aliwasili akiwa na gari lake ,alipaka gari na kuingia kazini ,kila mfanyakazi alimwangalia vanesa kwa hofu na kutetemeka kwani Vanesa alikuwa ni mzuri sana mbali na uzuri alikuwa na akili na uwezo kupindukia ,watu husema Mungu hampi mtu vyote ila kwa Vanesa ni kama alijaliwa vyote

Vanesa aliingia moja kwa moja alikabidhiwa taarifa na kuanza kazi ,alikaa kitengo cha kukagua taarifa na kurekodi mapato ya kampuni

Ilipofika mchana wafanyakazi waliingia na kumpatia taarifa za kila kitengo Vanesa alikuwa akizikagua na kujaza ,

Baada ya miezi mitatu kupita ,Vanesa alipandishwa cheo na kuwa meneja wa kampuni ,hakuna rangi ambayo wafanyakazi hawajaona ,Vanesa hakuwa na huruma kabisa ulikuwa ukikosea mara moja tu na kazi ndio umekosa

Siku moja majira ya saa tatu wafanyakazi wakiwa wameshawasili kazini aliingia mama mmoja ambaye alikuwa akijishughulisha na usafi  katika supermarket ile mama Yule aliingia akiwa anahema sana alipofika alikimbia na kushika vifaa vya usafi

Vanesa akiwa ofisini alimwona  kwa nguvu aliropoka

``Wewe nguruwe mwitu ndio unaingia kazini sasa hivi ? sheria inasema saa ngapi’’

Mama Yule alitetemeka kwa hofu na kumwomba Vanesa amsamehe amebanwa kwani anawatoto wadogo na mume wake ni mgonjwa

Vanesa alimtimua mama Yule kazi siku hiyo hiyo ,mama Yule alilia sana ila Vanesa alikuwa akicheka kwa dharau sana  wala hakumsikiliza .Ilipofika kesho asubuhi vanesa alitimua zaidi ya wakina dada kumi na wawili kutokana na kujipamba na kuvaa nguo fupi.,,Sababu hizi hazikuwa na msingi kabisa ila kutokana na wivu na kutaka kuonekana mwenye mamaka Vanesa alijikuta akifanya hivyo ,ndani ya siku hiyo hiyo waliletwa wafanyakazi wengine kwa ajili ya kufidia nafasi hizo

Heshima ilitawala mahali pale kila mmoja alikuwa akitetemeka mbele ya vanesa .,Vanesa aliogopeka kama Mungu kila mmoja alikuwa akimwogopa sana ,

Siku moja Vanesa akiwa anazunguka sehemu ya juu ya ghorofa za kampuni ile ,alikuwa anapendelea sana kupunga upepo huku akitazama kazi zinavyokwenda

Vanesa kwa mbali alimwona mzee wa umri wa miaka  65 akiwa anababaika huku akidondosha baadhi ya mizigo ,mzee Yule alipata shida kubeba mizigo hii ni kutokana na umri wake kuenda

Vanesa akiwa anamtazama ghafla mzee Yule alidondosha boksi kubwa lililokuwa limesheheni vikombe vyenye thamani ,Vanesa kwa haraka alishuka chini ,alipofika chini wafanyakazi wote walikuwa wakimpa pole babu ,walijua lazima hizi gharama zitakatwa kwenye mshahara wake kama ilivyokuwa kawaida

Mzee alilia kwa uchungu kwani maisha yake yalikuwa magumu mno

Kwa hasira vanesa alimgombeza ``Na wewe mzee umefanya upuzi gani’’

Mzee alipiga magoti ,Vanesa alimrukia na kumtandika makofi mazito mawili

Kila mfanyakazi alifunga macho maana hii ni dhambi ya kukufuru kumpiga baba yako

Vanesa aliropoka

``Vikombe hivi ni takribani laki tatu mshahara wako ni laki mbili na nusu sasa kuanzia sasa hudai kampunin kitu zaidi sana sisi tunakudai ,unaona ule mlango pale hebu potea na usikanyage hapa hatukai na wazembe sisi’’

Wafanyakazi walinywea kimya ila wawili waliropoka na kusema

``Dada unakosea hatuendagi hivyo kwanza umekosea kumpiga baba yako’’

``Nimekosea sio sasa kufumba macho na kufumbua na nyie wawili nisiwaone ‘’

Walitimuliwa kazi wafanyakazi watatu siku hiyo akiwa pamoja na mzee Yule

Vanesa alikuwa habari ya mjini ,kutokana na urembo wake ,elimu yake kila mmoja alimwogopa wanaume waliogopa hata kumtongoza ,Vanesa alijikuta akiitembea na kuwa na mahusiano na mmiliki wa kampuni ile ambaye alikuwa ni baba mwenye familia yake na mke wake

Mke wa mkuu Yule alikuwa akilia sana kila siku kwa jinsi bwana ake alivyokuwa akimsaliti kisa Vanesa ,mama Yule alikuwa akimfuata Vanesa na kumwomba aache kufanya hivyo ila vanesa hakutaka kusikia zaidi sana alikuwa akimtukana sana mama Yule kwa majibu ya nguoni

``Mwone huyu na litumbo lako hilo nani akupende mwache bwana ako ale maisha ‘’

Mama Yule alilia sana na kumwambia Vanesa Mungu yupo  na atakulipa tena mapema kabisa

Dharau za vanesa zilikithiri kila mfanyakazi alikuwa amechoshwa sio wanaume wala wanawake vanesa alikuwa akiwazibua vibao kama watoto ,hakika hii iliwachafua kila mtu alikuwa akimlaumu ,wafanyakazi walipolalamika kwa mkuu wa kampuni ndio kabisa hakuwasikiliza kwani alikuwa amekufa na kuoza kimapenzi kwa Vanesa

SIku moja Vanesa akiwa anakagua baadhi ya mazingira ya supermarket ile alipanda na kusogea juu kabisa ghorofa ya nne ya jingo lile ,akiwa anakanyaga ngazi kiatu chake kilicheza alishindwa kabisa kujizuia alijitahidi kujishikiza na chuma ila hakuwa na mazoezi ,huwezi amini Vanesa alidondoka kutoka ghorofa ya nne hadi chini ,kilichosikika ni kilio kimoja tu

Wafanyakazi walikimbilia kuona kunanini ,kila mtu alishangazwa na alichokiona ,Vanesa alivunjika mkono wa kulia ,miguu alivyodondoka nayo ilitua chini hivyo ilivunjika kama pingili za miwa ,ama kweli kama wewe ni mwoga usingeweza kutazama ,wafanyakazi walijikuta wakisema

``EEE mwanadamu kiko wapi kiburi chako ,iko wapi heshima yako ,kweli tuishi vizuri na watu’’

Kwa haraka alichukuliwa na kupelekwa hospitalini hali yake ilikuwa mbaya mno alitibiwa .huwezi amini hadi mkuu wa kampuni baada ya kumwona Vanesa alivyoharibika mwili wake alimkimbia

Vanesa alikuwa kilema wa maisha alikatwa miguu yote miwili ,alijutia sana maisha yake ila hakuwa na lakufanya ,adhabu hio aliona ni kubwa sana alimtukana Mungu na kujuta kwanini hata amezaliwa ila vyote hivi havikusaidia

Imetungwa na,

Joshua shao

0622186752 sms/call

0713111547 whatsapp tu

 

       MWISHO

Jipatie simulizi mbili nzima kwa gharama ya sh 1000 pia utaungwa na kundi langu karibu sasa wasiliana nami kwa namba tajwa hapo juu


No comments

Powered by Blogger.